Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kupitia taarifa kwamba Tanzania ilifuata utaratibu uliopo kisheria na kwamba mataifa hayo mawili yamekuwa yakiwasiliana.
Waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohamed ameilalamikia serikali ya Tanzania kufuatia hatua ya taifa hilo.
''Tulidhani
kwamba mazungumzo ya kidiplomasia yangetatua mzozo huu, lakini
tulishindwa kuafikia makubaliano. Ni wakati huo ambapo tuliamua
kuzungumza na balozi wetu nchini humo kuwasilisha barua ya kupinga hatua
ya kuwapiga mnada mifugo hao''.
''Historia ambayo tumekuwa nayo
na Watanzania ni nzuri sana na kila kunapotokea tatizo tumekuwa
tukitatua.Ni kwa sababu hiyo ambapo imekuwa hatua ya kushangaza miongoni
mwa wafugaji wa Kenya'', waziri huyo alizungumza katika mkutano na
vyombo vya habari.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri
kwamba Serikali ya Kenya ilimwita balozi wa Tanzania aliyeko Nairobi
kutaka maelezo zaidi.
"Balozi wetu alisikiliza maelezo ya Serikali
ya Kenya na akatumia fursa hiyo kuelezea masuala haya kwa Serikali ya
Kenya. Vile vile Serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu
masuala haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi,"
taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imesema.
"Serikali inapenda kuufahamisha umma kwa ujumla kuwa
uingizwaji wa mifugo na bidhaa zake nchini Tanzania huongozwa na sheria
za nchi, makubaliano ya kikanda na kimataifa."
Tanzania imesema
kuwa ilipobainika kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya mifugo kutoka nchi
za jirani wameingizwa nchini humo pasipo kufuata sheria na taratibu
zilizopo, serikali iliagiza mifugo hiyo irudishwe kwenye nchi kusika.
"Serikali
ilitoa muda wa kutosha kwa wamiliki wa mifugo hiyo kuiondoa nchini.
Tahadhari ilitolewa kwamba muda uliotengwa ukifikia ukomo, mifugo hiyo
itakamatwa na kushugulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi," taarifa hiyo
imesema.
Aidha, wizara hiyo imesema Waraka wa Kidiplomasia
ulitumwa kwa kwa Serikali za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda,
ikizihimiza kuwataka raia wao walioingiza mifugo nchini isivyo halali
waiondoe.
"Wamiliki wengi walitii agizo hilo la Serikali ya Tanzania na kuondoa mifugo yao nchini.
No comments:
Post a Comment