Tuesday, 22 May 2018

MLINDA MLANGO WA TIMU YA CHELSEA ATOA MASHARTI MAKALI ILI KUBAKI CHELSEA MSIMU UJAO


Mlinda mlango mahiri wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Thibout Coutors, ameuambia uongozi wa Chelsea kama wanataka abaki basi wahakikishe wanafanya usajili mkubwa na katika dirisha hili la usajili.
Coutors anayesifika kwa umbo la urefu, ametoa masharti hayo baada ya kuona mambo hayaendi vizuri ndani ya kikosi hicho huku akiitaka Chelsea kuwekeza kama Manchester United na Manchester Ciry.
"Tutajua baada ya Kombe la Dunia kama nitabaki hapa au nitaondoka ila ili nibaki ni lazima wafanye usajili mkubwa wa kueleweka"
"Lazima tuwaangalie Manchester United na Manchester City walivyowekeza na kupata mafanikio hivyo tutajua baada ya michuano ya Kombe la Dunia na hivyo kazi ipo kwa uongozi kuamua kufanya usajili au waache" 
Coutors anawindwa vikali na wakali wa Real Madrid pamoja na Atletico Madrid ambako aliwahi kucheza kwa mkopo zaidi ya msimu mmoja.

No comments:

Post a Comment

KASUMBAI