Washambuliaji Lionel Messi, Sergio
Aguero, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain wamejumushwa katika kikosi cha
wachezaji 23 watakaoiwakilisha Argentina kwenye kombe la dunia nchini
Urusi
Lakini mfungaji bora zaidi wa ligi ya Serie A mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi ameachwa nje.
Aguero anajiunga na wachezaji wengine watano wa Premier League akiwemo wanayecheza pamoja huko Manchester City Nicolas Otamendi.
Argentina wataaza mechi za Kombe Dunia dhidi ya Iceland tarehe 16
Juni kabla ya mechi zingine dhidi ya Croatia na Nigeria katika kundi D.
Nusura
watupwe nje ya Kombe la Dunia lakini hat-trick ya mshambuliaji wa
Barcelona Messi iliwaokoa wakati wa mechi yao ya mwisho ya kufuzu.
Kikosi kamili cha Argentina Hiki hapa
Walinda lango: Sergio Romero (Manchester United), Willy Caballero (Chelsea), Franco Armani (River Plate).
Walinzi: Gabriel
Mercado (Sevilla), Federico Fazio (Roma), Nicolas Otamendi (Manchester
City), Marcos Rojo (Manchester United), Nicolas Taglafico (Ajax), Javier
Mascherano (Hebei Fortune), Marcos Acuna (Sporting Lisbon), Cristian
Ansaldi (Torino).
Viungo wa kati : Ever
Banega (Sevilla), Lucas Biglia (AC Milan), Angel Di Maria, Giovani Lo
Celso (wote wa Paris St-Germain), Manuel Lanzini (West Ham), Cristian
Pavon (Boca Juniors), Maximiliano Meza (Independiente), Eduardo Salvio
(Benfica).
Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain, Paulo Dybala (both Juventus), Sergio Aguero (Manchester City).
No comments:
Post a Comment