Sunday 19 November 2017

WANANCHI WA ZIMBWABWE WAMTAKA MUGABE AACHIE NGAZI


Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.

Waandamanaji nchini Zimbabwe wameelekea katika afisi ya rais Mugabe ili kumtaka kujiuzulu.

Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.


Waandamanaji wakiunga mkono jeshi
Image caption Waandamanaji wakiunga mkono jeshi

Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980.
Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni.
Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu -PF.
 
Wapiganiaji wa uhuru ambao hadi kufiki mwaka uliopita walikuwa watiifu kwa rais Mugabe pia wanasema kwamba rais Mugabe anafaa kung'atuka mamlakani.
Kiongozi wa shirika hilo amewataka raia kuelekea katika makao ya rais Mugabe.
Nje ya ikulu ya rais kuna baadhi ya watu walioketi chini ili kuonyesha pingamizi yao mbele ya majeshi, huku kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai akihutubia umati mkubwa.

No comments:

Post a Comment

KASUMBAI