Thursday 16 November 2017

HALI YA UKIMYA YAZIDI KUTANDA NCHINI ZIMBABWE





Kufuatia kile kinachodaiwa kuwa ni mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Jeshi nchini Zimbabwe, hali ya ukimya na sintofahamu imezidi kuwaumiza kichwa wananchi wa nchi hiyo. Hali ya wasiwasi ya sasa ilianza kuzuka juma lililopita wakati rais Robert Mugabe alipomfukuza naibu wake Emmerson Mnangagwa na kumshutumu kwa kutomtii na kupanga kutwaa madaraka.

Wakati hali hiyo ikiendelea, wananchi wameendelea na shuguli zao za kila siku huku jeshi likiendelea kuweka doria katika maeneo muhimu mjini Harare. Hayo yanaendelea wakati ujumbe maalum kutoka jumuiya ya SADC ukiwasili nchini Zimbabwe kujadili kwa pamoja na Rais Robert Mugabe kuhusu hali ya baadae ya nchi hiyo.

 Mwenyekiti wa SADC ambaye ni Rais wa Afrika kusini Rais Jackob Zuma, amesema ni mapema mno kuzungumzia mustakabali wa hali ya kisiasa nchini Zimbabwe huku Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini humo kutoka chama cha  Movement for Democratic Change (MDC),  bwana Morgan Tsvangirai akisema kuwa matatizo makubwa ya kitaifa nchini zimbabwe yanahitaji suluhisho la kitaifa na Jumuiya ya Kimataifa.




No comments:

Post a Comment

KASUMBAI